Hugoline Martin Mtambachuo au unaweza kumuita DJ CHOKA aka Mr Appetite baada ya kukaa kimya kwa muda wa mwaka mmoja bila kuendelea na mix tape zake, mwaka huu amehamua kurudi tena.
Dj Choka anasema alikuwa kimya mwaka 2014 kwa kuwa alikuwa busy akimlea mtoto wake na familia yake, wimbo wa mwisho kuutoa ulikuwa unaitwa STINGA LI ambao ulikuwa umetengenezwa na Prod Pancho Latino kutoka Bhitz Music Group.
Mwaka huu 2015 Dj Choka anaanza na wimbo wake wa kwanza alioupa jina la NITALALA UZEENI huku akiwa amewashirikisha wasanii kama Country Boy, Climax Bibo, Young Lunya, Bgway na Deddy. Wimbo huu umesimamiwa na Prod mchanga anayekuja vizuri anajulikana kwa jina la GARD kutoka A.M Record.
Wimbo huu unatarajiwa kutoka siku ya Ijumaa tarehe 13 mwezi huu wa 3, na matarajio ya video yako mbioni kufanyika na kampuni ya utengenezaji video kutoka hapa hapa Tanzania.
Pichani ni Dj Choka akiwa na Deddy
Pichani kuanzia kushoto ni Prod Gard, Prod Maneck na Dj Choka wakiwa studio ya A.M Rec
Dj Choka, Deddy, Young Lunya & Prod Gard
Twitter: @djmwanga
Instagram: @djmwanga
Facebook Fans Page: DJMwanga