NAVY KENZO | ALBAMU MPYA ILIOSHIRIKISHA WAIMBAJI KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI

NAVY KENZO YATANGAZA: ALBAMU MPYA ILIOSHIRIKISHA WAIMBAJI KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI

Navy kenzo, Kikundi cha mziki wa dancehall kutoka Tanzania wametangaza kwamba albamu yao ya pili itabeba jina la “Story of The African Mob” na itapaitkana kwa manunuzi ya awali kwanzia tarehe 24 Julai 2020 kwenye jukwaa za Apple music, Spotify, Tidal na Deezer.

Albamu hiyo yenye nyimbo 12 inasherekea utofauti wa watu wakiafrika haswa ukizingatia mavazi yao, sanaa zao, miziki wao na jinsi wanavyosherkea utamaduni wao.

Kikundi cha Navy Kenzo kimeundwa na watanzania wawili Aika na Nahreel. Aika ni fundi wa kuandika mashahiri na Nahreel ni mtaalam wa kutengeneza biti za mziki. Baada ya miaka mingi ya kushibana kirafiki na kimahusiano, wawili hao wakaamua kujaribu bahati yao kwa kuungana kimziki na kuanzisha kikundi cha Navy Kenzo. Ili lipa. Wawiili hawa walithibitisha kuwa kama wanatisha kwenye tasnia ya mziki Kikundi kilichopata mafanikio mengi na kuanza kujulikana barani Afrika baada ya ngoma yao kali ya Chelewa na kuendeleza mafanikio hayo kupitia nyimbo zilizobamba kama vile Kamatia, Game, Fella na Katika wimbo wao na Diamond Platnumz. Walikuwa wamesha beba heshima kubwa kimziki kabla hata ya kutoa albamu yao ya kwanza 2017 iliokuwa na nyimbo zilizo fanya vizuri kama vile Bajaj iliomshirikisha Patoranking na Morning.

Story of the African Mob ni album inayoshirikisha waimbaji mashuhuri kutoka barani Afrika. Wakiwemo Nandy the African Princess, Tiggs da Author ambaye ni Mtanzania mwenye makazi Uingereza na mastaa wanaokubalika kutoka Ghana kama; King promise, Mugeez na MzVee. Navy Kenzo pia wameonyesha juhudi za kuinua vipaji kwa kushirikisha waimbaji wapya Eddy the Great na Genius Jini, alieyibuka mshindi wa Why Now competition ilioandaliwa na Navy Kenzo na Audiomack.

Navy Kenzo pia wametangaza kwamba wataachilia ngoma ya Bampa 2 Bampa iliomshirikisha Nandy tarehe 31 Julai 2020 na ngoma ya Pon Mi iliomshirikisha Tiggs Da Author tarehe 14 Agosti 2020.

Albamu nzima itapatikana kuanzia tarehe 4 Septemba 2020 katika jukwaa zote za mziki. Mashabiki wajitayarishe kuburudika na mchanganyiko wa ladha za kiafrika na kijamaika zilizotengenezwa na Nahreel akishirikiana na maproducer wenzake. Waliofanyia kazi katika albamu hii ni pamoja na Mantra na JuwonMix kutoka Marekani, Buskillaz kutoka Israel, Killbeatz kutoka Ghana na Pablo Lannoche, Breezy beatz na Chizan Brain kutoka Tanzania.

Navy Kenzo wanasema kwamba wamebarikiwa kuweza kuongelea hisia zao kupitia mziki na kupata nafasi ya kutengeneza album hii imewahamasisha kuwa na moyo wa kutoa kwa Watanzania wenzao. Mashabiki wao wana shauriwa kufuatilia account zao za mitandao ya kijamii ambapo watatangaza zawadi watakazo gawa hivi karibuni.

Kwa taarifa zaidi kuhusu Navy Kenzo na albamu ya “Story of the African mob” jiandikishe kwenye ukurasa wao wa youtube TheNavyKenzo na tembelea Instagram @navykenzoofficial and Twitter @Navykenzo

Linki ya ku pre-save> http://africori.to/sotam