FAQ

Karibu Katika MASWALI na MAJIBU Kuhusu Website Yetu!

Baadhi Ya Watu Huuliza!

1: DJMwanga.com ni Tovuti ya Namna Gani?

JIBU: DJMwanga.com ni tovuti ambayo inaweka kazi za wasanii ili ziweze kuonekana kwa watembeleaji kupitia Kutafuta kwenye Google, Yahoo, Yandex na kwenye mitandao mingine ya kutafuta Vitu (Search Engine)

2: Nawezaje kuweka wimbo wangu ukaonekana kwenye Webste ya DJMwanga.com?

JIBU:  Tunapokea nyimbo kupitia Email au WhatsApp “MAWASILIANO

3:  Je naweza Kutuma Nyimbo kupitia WhatsApp?

JIBU: Ndio unaweza kutuma kupitia WhatsApp [utume kama Documents (Nyaraka)]

4: Je ni Nyimbo za aina gani Naweza Kutuma DJMwanga.com?

JIBU: Tunapokea Mahadhi ya nyimbo zote (Lakini ziwe na Maadili Katika Jamii) ikiwa ni pamoja na picha ,video na sauti kutoka kwa wamiliki au wawakilishi walioidhinishwa ambao wanamiliki haki zote.

5: Je Kuna Malipo yoyote ya Pesa Msanii hupata akiweka Nyimbo Zake Kupitia DJMwanga.com?

JIBU: HAPANA , DJMwanga.com inawapa watembeleaji Kutazama Video bure, upakuaji wa sauti au utiririshaji/Kusikiliza.  Hii inamaanisha kuwa, huduma zetu zote ni Bure kwa dhumuni la Kutangaza na kuendeleza Kazi za Wasanii na kwa hivyo hatuuzi muziki wa msanii, video au picha yoyote kwa mtu wa tatu.

6: Je Nikiweka Wimbo Wangu Mtu Anaweza Kutazama Au kusikiliza na watazamaji wakaongezeka kwenye Akaunti yangu? Mfano Youtube Au BoomPlay na Audiomack!

JIBU: NDIYO, Wimbo wa Msanii unapowekwa kwetu iwe Video au Sauti , Basi huwa tunanakiri upachikaji (Embed Code) kutoka kwenye Akauti ya msanii ambayo ipo kwenye tovuti za watu wengine. Mfano kusikiliza kutoka BoomPlay, Audiomack, Youtube na tovuti zingine ambazo zina huduma ya Upachikaji (Embed Code).

Zingatia: Hatuhusiki na tovuti za watu wengine kama BoomPlay, Audiomack, Youtube N.k kwa namna yoyote ile iwe kuhesabu watembeleaji au kuhusu malipo yanayofanyika huko, Hatudhibiti yaliyomo au viungo vinavyoonekana kwenye tovuti hizi na hatuwajibiki kwa namna yoyote ile na wavuti zilizounganishwa kutoka kwa Tovuti yetu, Kama inavyojieleza Kwenye Kipengele cha Sera ya faragha (Privacy Policy) aya ya Third party websites.

7: Je nawezaje Kutoa Wimbo wangu ambao umetumwa na mtu ambaye Hana hakimiliki?

JIBU: Kama umeuona wimbo wako ambao hujapenda uwepo kwenye tovuti yetu, Tunakuomba utume maelezo au malalamishi ya kutaka kuondoa wimbo wako kupitia Email ya [email protected] na mafundi wetu wataweza kuondoa kazi yako ndani ya Masaa Kadhaa ikiwa tu watajiridhisha kuwa una haki zote za wimbo huo.

NYONGEZA

ZIJUE BAADHI YA FAIDA ZA KUWEKA WIMBO WAKO DJMwanga.Com

  •  Wimbo wako utaonekana Kwenye Mitandao yote ya Kutafutia Vitu Mbalimbali kama Google , Bing , Ask , Yahoo na Mitandao mingine inayotumika Katika Utafutaji Vitu Mtandaoni na kufanya wimbo wako kujulikana zaidi.
  • DJMwanga.com inatazamwa Zaidi ya mara 10M+ nakuendelea kwa Mwezi Mmoja.. Hivyo basi wimbo wako utaonekana kwa Watembeleaji wengi pia.
  • DJMwanga.com ina sehemu ya Kushare/Kusambazia Muziki wako kama Facebook , Twitter na Mitandao mingine ya kijamii ambayo unaweza kutumia kwa Kuwasambazia Marafiki na jamaa.
  • Mtembeleaji wa tovuti yetu ataweza Kudownload au kusikiliza Wimbo wako kwa urahisi Zaidi Kupitia Player ambazo zimeambatanishwa na akaunti yako kutoka mitandao ya kulipia Kama Audiomack, Youtube, BoomPlay n.k.

Pia Kwa Maelezo ya Ziada Unaweza Kusoma Kwenye Kipengele cha Sheria na Masharti (Terms & Conditions)

Kama una Swali lolote usisite Kutuuliza Kupitia Email Yetu [email protected].

Asante!.