Mbooso, amedondosha rasmi ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la “Pawa”, ikiwa ni wimbo wa kwanza kwenye EP yake mpya yenye nyimbo 7, chini ya lebo yake mpya kabisa – KHANMUSIC.
Katika ngoma hii, Mbooso anatuletea simulizi tamu la mapenzi, akiwa anamuelezea mpenzi wake kama chanzo cha nguvu, faraja, na msukumo katika maisha. Kwa sauti ya upole iliyojaa hisia, mashairi yake yanafika moja kwa moja moyoni:
“Kamusi namaliza kurasa kukusifia,
Kama penzi ni chupa ya bia – nipe sana niwe mlevi…”
Ni mistari ya kipekee inayovunja mipaka ya kawaida ya uandishi wa mashairi ya muziki wa Bongo Flava. Mbooso haishii hapo – anazidi kuonyesha namna mpenzi wake ni dira na msaada wa maisha:
“Ni yumbe yumbe njia, kwa maana we mlezi na unanijulia,
Pawa pawa, naishiwa pawa, penzi lako mizani nzito – naishiwa pawa…”
Ngoma hii imekuja na miondoko laini yenye ladha ya Afro-Bongo, ikiwa na production safi inayomtoa Mbooso kwenye ngazi ya msanii wa kawaida hadi kuwa sauti ya kupasua anga.
PAWA: Mwanzo wa Safari Mpya
“Pawa” si tu wimbo wa mapenzi – ni ishara ya mwanzo mpya kwa Mbooso. EP hii mpya inaonekana kuja na maudhui ya kina, na “Pawa” imefungua milango kwa mashabiki kutarajia ngoma nyingine kali zenye hadhi ya kimataifa.
Kwa mashabiki wa muziki wa mapenzi, huu ni wimbo wa kuuweka kwenye repeat. Ujumbe, sauti, na hisia – vyote vimekamilika!
Mbosso level nyingine aisee👐
kaka upo vlz sana enderea kutupa buludan tuna enjooy sana