Rockies models, kampuni mpya ya urembo iliyoanzishwa jijini Mwanza imeanza kwa mshindo mkubwa na kuwashitua wengi ndani na nje ya jiji la Mwanza. Mwanza ililipuka kwa shangwe na mayowe jana katika ukumbi wa JB Belmonte hotel uliopo katikati ya jiji la Mwanza wakati warimbwende hao wakikatiza jukwaani kwa mwendo wao maarufu kama CATE-WALK.
Kama haitoshi warembo hao walishangaza wengi kwa vipaji walivyonavyo kwani mbali na uzuri wa sura zao warembo hao ni wakali wa fani nyingine kama kuimba, kudance, kuigiza nk.
Tukio hili ilishuhudiwa na wadau kibao kutoka makampuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Twitter: @djmwanga
Instagram: @djmwanga
Facebook Fans Page: DJMwanga