Donny Flavour Ft. Mr Blue Coming Soon

Msanii wa mziki wa Bongoflava Donny Flavour Ameamua kuvunja ukimya na kurudi kwa kishindo baada ya kuachia ngoma ya twende nyumbani na sasa anakusogezea ngoma yake mpya ambayo amefanya na rapa mkali kutokea Tanzania namzungumzia Mr Blue Kabyser ngoma inaitwa ”Ameniweza”

Akizungumzia kuhusu ngoma hiyo Donny amesema toka muda mrefu alitamani kufanya ngoma na Mr Blue lakini uongozi wake  ulimuambia asubiri ili kuipisha ngoma ya Twende nyumbani kufanya vizuri zaidi na kuipa promo na nashukuru baada ya Twende Nyumbani ngoma mpya  inafata ambayo nimezungumzia mapenzi katika namna ya kipekee sanaa ambayo wadau naamini wataipokea vizuri sana,Amesema amemshirikisha mr blue kwasababu ni rapa ambaye anajua kuandika na anauwezo mkubwa wa kuandika na kubadilika.

Aidha amezungumzia kuhusu mipango yake amesema kuwa tayari kuna Tour ambayo inakuja baadhi ya mikoa ya Tanzania itahusika katika Tour hiyo na ameeleza kuwa ngoma ya Ameniweza  imetengenezwa na producer Tony Drizy katika studio za Kaburu Musics Records huku akisema anaimani kubwa na mkono wa Tony.

Pia amewashukuru wadau wake kwa support kubwa wanayompa na wakae tayari kwaajili ya kuipokea ngoma hii mpya ambayo itatoka pamoja na video mwezi huu wa tatu na Kuhusu video Donny amepanga kufanya na Director Nick Classic wiki ijayo.

Pia amemshukuru waziri wa habari sanaa  utamaduni na michezo Nape Nnauye kwa kuwapa moyo wasanii na mipango yake katika kukuza sanaa ya Tanzania inampa Moyo mkubwa wa kuzidi kufanya vizuri kimataifa zaidi,Ameushuru uongozi wake kwa kutoa support kubwa katika mziki wake. 
Aidha amesema kuna ngoma nyingine  itakuja ambayo hajataka kuweka wazi sana  atafanya na msanii mkubwa ila kwa sasa yuko nchini marekani na akirudi Uongozi wake utakaa naye chini na kujadili 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *