Rayvanny Kuachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni.

Msanii wa muziki kutoka WCB, Rayvanny amedai ataachia wimbo wake mpya muda mchache baada ya kutoka kwa video ya wimbo ‘Kijuso’ alioshirikishwa na Queen Darlin.

Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta Kiki’ amedai ameandaa kazi nyingi ambazo zinasubiri wakati wa kutoka.

Akizungumza na mashabiki wake live katika mtandao wa Instagram (Insta Live) Jumanne hii, Rayvanny amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kazi mpya.

“Mashabiki wangu soon nitaachia wimbo mpya, sema itaanza kwanza kutoka video ya ‘Kijuso’ na baada ya hapo ndo mzigo unaweza kutoka,” alisema Rayvanny.

Muimbaji huyo toka aachie wimbo ‘Natafuta Kiki’, ameshirikishwa kwenye ngoma zaidi ya 3 ambazo ni pamoja Salome aliyoshirikishwa na Diamond, Kijuso na Queen Darlin pamoja na Mugacherere na Q Boy.

JIUNGE NAMI KUPITIA