Sababu ya Wasanii kukataa kulipwa na kuikataa COSOTA


Kupitia #PLANETBONGO @nikkwapili ametoa ufafanuzi kuhusu wasanii
kutoa mapendekezo kusitisha mpango wa kulipwa mirabaha na mapendekezo ya
kuvunjwa kwa bodi na management ya chama cha hatimiliki Tanzania
#COSOTA .HAYA NDIYO ALIYOSEMA… -Kwanza taasisi iliyopewa tenda hiyo
#CMEA inamilikiwa na kampuni ya #PUSHMOBILE ambayo wasanii wameshuhudia
kua INA historia mbaya ya kuwaibia wasanii kwahyo hawawez kuwaamini
tena. -Pili Sheria iliyounda #COSOTA inasema lazima iundwe na kusimamiwa
na wasanii wenyewe lkn haipo hivyo.kwahyo wasanii wanataka #SHERIA
ichukue mkondo wake na #cosota isimamiwe na iongozwe na wasanii.

Pia bodi ya COSOTA haiundwi na wasanii na pia #UTENDAJI wa COSOTA
siyo wa kurizisha ikiwemo kuwashauri wasanii issue za kimuziki ni jukumu
lao lkn hawafanyi hivyo. -Kingine ni mazingira ya ulipaji mirabaha
YANAONEKANA HAYAPO TAYARI.mfano wanasema Mziki utakaopigwa uwe wa nje au
ndani (_ya nchi)utalipiwa,wakati huo huo wanasema ili wimbo ulipiwe
lazima usajiliwe COSOTA na #CMEA ,lkn ukwel in kua nyimbo nyingi za nje
na za nyumban hazijasajiliwa Popote kati ya taasisi hizo. -Kadhalika
wanasema #MAUDHUI ya #Media za nyumbani 60% nyumbani na 40% ya nje na
sheria hii imekuwepo kwa miaka mingi lakini ukiangalia uhalisia hasa kwa
vituo vya #Tv hapa Bongo maudhui yake 80% ni ya nje.
Kwamaana hiyo usimamizi huo haupo na wasanii hawawezi kusaini na
kukubalina na mambo yasiyokuwepo kiuhalisia. -mwisho Ukiangalia hii
sheria wanasema ni makubaliano ya kiukanda wa #AfricaMashariki kuwa
media zipige 60% local content lakini ukiangalia #kenya mambo ya
mirabaha yalipoanza media zilianza kupiga 80% maudhui ya nje na kwahyo
hii sheria haina #Uhalisia.

JIUNGE NAMI KUPITIA 
Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *