Msanii wa muziki kutoka label ya Wema Sepetu, Endless Film, Mirror anajipanga kuachia kolabo yake na Ommy Dimpoz.
Meneja wa msanii huyo kutoka
Endless Film, Petitman Wakuache, amesema Mirror ni msanii ambaye style
yake ya uimbaji haiwezi kufananisha na wasanii mwingine.
“Mirror ni msanii mzuri sana na muziki wake hauwezi kuufananisha na
wa wasanii wengine, kwa hiyo watu msione kimya, kuna kolabo mpya Ommy
Dimpoz itatoka, pia kuna video mpya ambayo tumeshoot Afrika Kusini. Kwa
hiyo mashabiki wasione watu hawafanyi kazi, wakati kazi wanaziona, wao
wanatakiwa wasupport kazi zilizopo kwanza,” alisema Petit.
Pia Petit alisema Mirror ni msanii ambaye hauwezi kumfananisha na wasanii mwingine, kwani muziki wake unaishi muda mrefu.