Picha: AY akiwa ikulu ya Marekani na wasanii wengine wa Afrika

 AY amepata Nafasi Ya Kuingia ikulu ya Marekani kupitia mualiko maalum
wa Rais Obama kwa wasanii wa Afrika ambao walikuwa katika One Campaign
yenye lengo la kuhamasisha kilimo Afrika.

AY ameungana na wasanii wengine wa Afrika akiwemo Femi Kuti, D’Banj, Fally Ipupa, Victoria Kimani na Owamuni.

Waimbaji hao wanaungana na mchezaji wa Manchester City, Yaya Toure
jijini Washington D.C, mkutano ambao umeanza August 4 na utakamilika
August 7
.

Kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya
Marekani
pamoja na wajumbe wa Young African Leaders Initiative (YALI).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *