Download | Play Now

Diamond Platnumz azidi kupanda daraja, Sasa kuwania BET Award kipengele cha Best International Act: Africa

Ilikua stori kubwa pale Diamond Platnumz alipotangazwa kushiriki kwenye
tuzo za MTV Base (Mama Awards) kikiwa ni kituo kingine kikubwa cha
burudani Afrika.

Leo hii Diamond Platnumz ameingia kwenye stori nyingine kubwa ya dunia
baada ya kuchaguliwa kushiriki kwenye tuzo za Television kubwa ya
Marekani ya BET ambapo yupo kwenye kipengele cha wanaogombea BEST
INTERNATIONAL ACT AFRICA.

 Anaigombea hiyo tuzo na Davido wa Nigeria, Mafikizolo wa South Africa, Tiwa Savage wa Nigeria, Toofan na Sarkodie wa Ghana. the OFFICIAL nominees 2014!….

BET kupitia page yao ya twitter waliandika kuthibitisha kuchaguliwa kwa
Diamond na kumpongeza akiwa pia ni msanii pekee wa Afrika Mashariki
kwenye tuzo hizi za mwaka huu.