Jokate, Brown Mauzo, Abdu Kiba na wengine kuanza kuachia kazi chini yalabel ya Alikiba Music

Alikiba ametaja wasanii ambao wapo chini ya lebel yake ya ‘King’s Music”

Alikiba amewataja Jokate, Abdu Kiba, Delila, Abby Skills na Brown Mauzo wa Kenya kuwa ni baadhi ya wasanii ambao wapo chini ya label yake ambayo ameedai ipo tangu siku yingi lakini hakuitangaza tu.

“Mimi Record label ninayo muda mrefu,muda mrefu sana lakini sikufanya matangazo lakini nina wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi nimerudi tena najipanga upya nao waendelee kufanya kazi, kama ambavyo unamuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea kufanya kazi, pia kuna Abdu Kiba”  Alikiba alifunguka kwenye 255 ya Clouds Fm.

“Afu vilevile kuna msanii mwingine ambao watu hawajawahi kumsikia, Pia kuna wakiana Jokate, kina dalila na wengine wengi wapo chini ya label yangu, sijafanya rasmi lakini mtawasikia.”