hayo aliyo ulizwa ni Nini msimamo wake kuhusu Muziki wa singeli kuua Bongo fleva?
Ali Kiba
“Napenda sana Muziki wa Singeli, naaaaa endapo nitaufanya muziki wa singeli nitatumia lugha ya kistaarabu sana, yeaaa sisemi kwamba lugha ambayo wanaitumia sio ya kistaarabu ? aaaaaahhh
namaanisha kuwe na staha kidogo kwenye lugha inayotumika katika singeli, Naupenda sana muziki wa Singeli na sasa hivi umepata sapoti kubwa sana, kwa kila rika kwa sababu watu wana understand muziki yaani muziki yaani muziki hauna ujanja utaupenda tuu” alisikika akijibu swali hilo aliloulizwa na shabiki yake.
Hakuishia hapo aliendelea kujibu swali hilo kwa kusema “Mama yangu mimi anapenda sana muziki na katika muziki anaoupenda Singeli pia anaupenda, lakini kuna lugha ambazo zinatumika kwenye singeli, mama yangu hawezi kutumia, ili muziki wao uweze kukua zaidi kwani unapendwa sana”