New AUDIO | Mzungu Kichaa ft Juma Nature – Together As One | Download

Mzungu
Kichaa atoa single yake ya pili kutoka kwenye CD yake mpya iitwayo
RELAX. Katika wimbo huu amemshirikisha Juma Nature na Karen Mukupa.
Mzungu Kichaa alikuwa na haya ya kusema, “Juma Nature ndiye aliyenipa
jina langu la kisanii nilivyokuwa nikifanya featuring kwenye nyimbo
kadhaa za Bongo Flava mwaka 1999 na 2000. Pia niliweka vocals pamoja na
TID kwenye wimbo wa Nature uitwao Hili Game. Kwahiyo nina furaha kubwa
kupata fursa ya kufanya kazi na Juma Nature 
tena katika
wimbo hii. Karen Mukupa pia alishawahi kushirikiana na Nature siku za
nyuma na ni rafiki yetu sote wa siku nyingi. Karen ni msanii mkubwa sana
nchini Denmark anapotokea na nimefurahi kuweza kuwashirikisha wote
wawili
.” Mzungu Kichaa pia alisema kuwa wimbo huu ni kwaajili
ya kujenga umoja ili kufikia malengo na ndoto katika fani ya muziki.
Wimbo huu unazungumza kwa niaba ya wasanii wote wa Afrika Mashariki.


Vocals
zimerekodiwa studio ya MJ Records na ngoma zimerekodiwa live ndani ya
Caravan Records na Abdalla Membe, Shabani Rashid (keyboard), Kevin
Mpangala (Bass), Mzungu Kichaa (Guitar).
http://bit.ly/togetherAsOne