Download | Play Now

Video ya ‘Nje ya Box’ Ya Weusi Yaanza Kuoneshwa Channel O

Baada ya kuzungumzwa sana na kusifiwa hapa nchini huku ikichezwa mara
kwa mara na vituo mbalimbali vya runinga Tanzania, hatimaye video ya
wimbo wa kundi la Weusi ‘Nje ya Box’, imechezwa katika moja kati ya
vituo vikubwa vya runinga, Channel O.
www.djmwanga.com
 Video ya Wimbo wa Nje ya Box iliyofanywa na Joh Makini, Nikki wa Pili na
G-Nako, iliongozwa na Nisher, na story yake iliandikwa na Joh Makini.
Hii inakuwa video ya kwanza ya Weusi kuchezwa katika kituo hicho, lakini
pia kwa mujibu wa Joh Makini ndi video yenye gharama kubwa zaidi kuliko
video zote za Weusi.