Weka mbali na watoto, video ya Zigo Remix ya AY aliomshirikisha Diamond Platnumz, ruksa kuchezwa usiku kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA.
TCRA imetoa taarifa hiyo kwenye mtandao wa Twitter wakati ikijaribu kumwelewesha AY pamoja
mashabiki wenye duku duku kuhusiana na uamuzi huo. Awali uamuzi wa TCRA
ulitafsiriwa kuwa video hiyo yenye views zaidi ya milioni 2.7 Youtube
imepigwa marufuku kabisa kuoneshwa kwenye TV za Tanzania
@TCRA_Tz @CloudsMediaLive video za nje tunaziona kwenye vituko vya ndani,nakumbushia sijajibiwa swali langu la maadili yapi niliyokiuka— LEGEND (@AyTanzania) February 22, 2016
@TCRA_Tz @CloudsMediaLive Okay,naweza kujulishwa maadili gani yaliyokiukwa ili next time tusiyavunje— LEGEND (@AyTanzania) February 22, 2016
@CloudsMediaLive @AyTanzania TCRA haina utaratibu kuwasiliana na wasanii kuhusu kazi zao. Barua iliandikwa kwa vyombo vya Utangazaji.— TZ Communications (@TCRA_Tz) February 22, 2016