Diamond Platnumz athibitisha kuwa mbioni kumrudisha Q-Chief kwenye Ramani

Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amejipanga kumrudisha Q-Chief kwenye ramani ya muziki baada ya uongozi wake wa QS Mhonda kushindwa kufanya hivyo licha ya kudai kutumia zaidi ya shilingi milioni 200 bila kupata faida

Kwa muda kulikuwepo na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kumsainisha msanii huyo mkongwe kwenye label ya WCB. Na sasa, ingawa hajasema kuwa amepanga kumsanisha kwenye label hiyo, Diamond amekiri kuwa kwenye mipango ya kufanya kazi na legend huyo.
“Unajua lengo langu kama mimi au sisi vijana wa sasa hivi tunajaribu kuona tunavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano, so tuko na maongezi na bro tunaangalia tunawezaje kufanya kazi kwasababu ni mtu ambaye kwanza mimi namfeel halafu ambaye namuamini,” Diamond ameiambia Dizzim Online.
“Ni mtu ambaye najua kabisa yaani akibonyeza button hii basi huu mji mzima umechafuka. Kwahiyo siwezi kuyaongea mengi sema Watanzania watuombee dua tunachokiplan kifanyike vizuri,” ameongeza staa huyo.
Naye Q-Chief alisema, “mimi nahisi project inayofuata Simba anahusika kwasababu ni mtu ambaye ameniita kwa ushauri nikiwa na QS, amemuambia vitu vingi vya msingi, yeye shahidi hapa, lakini kama ni mtu anayeelewa mdogo wake ameniita amesema nini mpaka mimi nimeelewa na hajafanya maybe [QS] is not ready to do business but Diamond is a business man and I am ready to join a business man so long as kuna misingi. Lakini naamini ngoma inayofuata Diamond amenipa baraka zake.”
Hivi karibuni muimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Abubakar Katwila amekuwa kwenye vita vya maneno na kampuni inayomsimamia ya QS Mhonda anayoishutumu kwa kushindwa kumfikisha popote licha ya uwekezaji mkubwa ilioufanya kwake.
Ndugu zake pia walihoji kuhusu mkataba wa maisha aliosainishwa mtoto wao kwenye kampuni hiyo na kwamba tangu awe chini ya kampuni hiyo hawajaona mabadiliko ya maana kwenye maisha yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *