Mashabiki wa Alikiba wamelala usingizi mnono baada ya kupewa habari
njema waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu. Video ya Lupela itaanza
kuchezwa leo kwenye kituo cha runinga cha MTV Base.
Kiba alitangaza habari hiyo njema kwenye Instagram Jumanne hii.
“I can’t wait ..Thank You @mtvbaseafrica #KingKiba,” aliandika kwenye
picha inayoonesha ratiba ya kuchezwa video hiyo iliyotoka wiki kadhaa
zilizopita.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya mashabiki wa Alikiba kuanza
kumshambulia meneja wake, Seven Mosha kwenye Instagram kutokana na hadi
sasa video hiyo kutooneshwa kwenye vituo vya kimataifa.
Haya ni baadhi ya malalamiko yao:
eng.allysm: @sevenmosha madam mbona mnatuangusha kwa Kiba mbona mambo
ayaendi km tulivyo Taraji please unaweza nipa sababu kwanini nyimbo za
Kiba azipigwi ktk TV za nje mf MTV na trace hasa lupela
alikiba_page: Video za alikiba azionyeshwi MTV na vtuo vingne vya
kimataifa why this happen ….inafika kipind tunachoka management yake
bhna ahaa
tamu_iwe_kavu: Ukweli usiopingika @sevenmosha mnamuangusha sana
@officialalikiba.. Hatuzioni ngoma zake zikipigwa katika stesheni
kubwa.. Hatuoni collabo za njee na wasanii wakubwa.. Mpo slow sana..
Sioni unavyompigania kiba kama unavyompigania jide.. Mnampotezea muda tu
kiba…. Mnaboa kusema ukweli..
masco_the_don_master: Oya kama kazi imewashinda mwachen kiba
tutamsimamia wenyewe coz haiwezekan lupela tokea imetoka haijapigwa
trace,mtv na vituo vingine vya kimataifa wakati now asilimia 70 ya
nyimbo za bongo mpaka za underground zinapigwa y kiba hapigwi???halafu
kwa nn collabo hazionekan? Halafu mmnachelewa xana kutoa nyimbo y kila
nyimbo baada ya miez 8??achen izo bhana mnamuua kiba halafu sisi ndio
tunaopata tabu mtaani so kama kaz hamuwez achen