YAMOTO BAND KUKWEA PIPA TAREHE 17 KUELEKEA UK

YAMOTO BAND KUKWEA PIPA TAREHE 17 KUELEKEA UK
 Kundi la Muziki wa Kizazi kipya Yamoto Band wanatarajia kuanza safari yao ya kwenda UK kufanya Show tarehe 17 mwezi huu na show itapigwa Tarehe 21 ndani ya Royal Regency.

Mkurugezi wa Kundi hilo Mkubwa Fella kwanza alianza kwa kutoa shukran zake kwa Mwenyezi Mungu, Mashabiki, Wadu na vyombo vyote vya habari kwa kuweza kutoa sapoti kwa vijana hao tangu walipo toa Kazi yao ya kwanza kabisa mpaka kufikia Leo wamepata mualiko mkubwa kabisa wa kwenda kufanya show UK, na kwa upande wa Msemaji mkuu na Kiongozi wa Band Aslay Isihaka amesema kuwa wanafuraha sana kwa kupata mualiko huo lakini pia wanashukuru kwa mungu, mashabiki na wale wote wanaonyesha sapoti katika muziki wao. Aslay amesema   kuwa watakwenda kufanya Kazi nzuri huko ili kuleta sifa ya muziki wa hapa nyumbani na hata heshima ya Taifa kwa ujumla.Kwa upande mwingine Vijana hao Wametoa shukrani zao kwa Viongozi wao Mkubwa Fella, Bab Tale, Chambuso, Mh Temba na Shirko kwa usimamizi Mzuri wa Kazi hizo.
Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *