Hii ni Nafasi Ya Pekee kwa Wasanii Chipukizi Kujaribu BahatiZoezi la wasanii kuchukua fomu za kushiriki kwenye tuzo za mwaka huu za EATV limefunguliwa Siku ya Jumanne.


Fomu hizo zinapatikana kwenye tovuti ya http://www.eatv.tv/awards 
Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.
Vipengele hivyo ni:
1. Mwanamuziki bora wa kiume
2. Mwanamuziki bora wa kike
3. Mwanamuziki bora chipukizi
4. Kundi bora la muziki
5. Video bora ya muziki
6. Wimbo bora wa mwaka
7. Muigizaji bora wa kiume
8. Muigizaji bora wa kike
9. Filamu bora ya mwaka
10. Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.
Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
https://goo.gl/Dpx8j4
JIUNGE NAMI KUPITIA 
Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *