Vitambue Vipengele 10 Vya Tuzo za EATV #EATVAwards2016

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Mkuu wa masoko wa kituo EATV, Roy Mbowe alisema tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.

Vipengele hivyo ni:
1. Mwanamuziki bora wa kiume

2. Mwanamuziki bora wa kike

3. Mwanamuziki bora chipukizi

4. Kundi bora la muziki

5. Video bora ya muziki

6. Wimbo bora wa mwaka

7. Muigizaji bora wa kiume

8. Muigizaji bora wa kike

9. Filamu bora ya mwaka

10. Tuzo ya heshima 

[itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki]

Mbowe amesema kazi za sanaa zitakazoruhusiwa kuingia kwenye vipengele ni zile zilizotoka kuanzia Julai 1 2015 – 30 Juni 2016. Tofauti na tuzo zingine, wasanii wanaotaka kushiriki watalazimika kujaza fomu za kutaka kutajwa kwenye tuzo na kuwasilisha kazi husika ambapo mchakato wa uchambuzi wa kazi hizo utachukua kipindi cha mwezi mmoja kabla ya majina yaliyoingia kwenye tuzo hizo kutajwa na kuanza kupigiwa kura.

Hata hivyo amedai kuwa pamoja na wananchi kupiga kura, kutakuwepo na jopo la majaji litakaloshiriki kupata washindi. Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

https://goo.gl/Dpx8j4
JIUNGE NAMI KUPITIA 
Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga

One thought on “Vitambue Vipengele 10 Vya Tuzo za EATV #EATVAwards2016

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *