Rich Mavoko – Ibaki Story | Lyrics/Mashairi

[Verse 1]
Matapishi ni kinyaa kuzirudisha tena kwenye kinywa
Japo mengi ulisema, kama nuru ghafla ukazima
Ikawa ngumu kukusahau, nikasema moyo ukome
Kwa kali sulu na madharau, penzi ulivunja na ngome

[Pre-Chorus]
Na unajua hata nikilia siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo
Aa ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani, ni ndoto
Wewe nirubuni kwa penzi la kidani kama mtoto

[Chorus]
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we
Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we
Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe

[Verse 2]
Kiliniumiza kitanda na shuka tuliolalia
Mapenzi yana siri kubwa, sishangai mtu akilia
Nimekubali mboni zangu zimtazame mwingine
Maridhia ya moyo wangu huenda si fungu pengine
Cha kushangaza hadharani mengi ya kuficha ukaweka wazi
Nikahisi sijui mapenzi, labda kwako sinogi nazi

[Pre-Chorus]
Na unajua hata nikilia, siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo
Aa ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani, ni ndoto
Wewe nirubuni kwa penzi la kidani kama mtoto

[Chorus]
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we
Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we
Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe

[Bridge]
Yalinitesa mazoea aya
Lakini mi nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya
Kidonda chake hakinaga dawa
Ee mazoea aah
Lakini mi nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya
Kidonda chake hakinaga dawa

[Chorus]
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we
Mapenzi mi na wewe, uuh uuh
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we
Mapenzi mi na wewe, uuh uuh

Download DJMwanga Android Application Click HERE

https://goo.gl/Dpx8j4
JIUNGE NAMI KUPITIA 
Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga