SARAH K,CHRISTINA SHUSHO,MARTHA MWAIPAJA KUIYUMBISHA ARUSHA LEO.

Unaweza kusema Arusha inaweza kutikisika Leo mara baada ya wasanii wakali wa nyimbo za injili kutoka Tanzania na Kenya watakapo kuwa wakihudumu katika Uwanja wa Shekh Amr Abed katika Tamasha la Upendo kwa MAMA.

Tamasha hilo lilokuwa likisubiriwa kwa Hamu kubwa na wakazi wa Mkoa huo na Viunga vyake sasa linakwenda kufanyika Leo ambapo kila mmoja anatarajia mambo mazuri kutoka kwa waimabji hao amboa wanaidadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa nyimbo za Injili.

Akizungumza na chanzo cha Habari hizi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya MKUNDI PRODUCTION ambayo niyo iliyohusika katika kuandaa tamasha hilo kwaajili ya kuwajali na kutambua umuhimu wa wakina mama,duniani kote Bw CARLOS MKUNDI amesema maandalizi ya Tamasha zima yamekamilika.

Amesema kuwa tayari wasanii karibia wote wamekwisha kuwasili ndani ya jiji La Arusha
Pia amesema anamshukuru Mungu kwakumpa kibali cha kuandaa tamasha kubwa la aina yake ambapo amesema jeshi la polis Mkoani hapa tayari limekubali kutoa Polis ambao watasaidia katika kusimamia na kulinda usalama wa watu wote ambao watahudhuria ndani ya Tamasha hilo.

Tamasha hilo litaanza majira ya saa 8 mchana na kiingilio kitakuwa ni Sh,3000 tuu,kwa kila mtu.

ad

One thought on “SARAH K,CHRISTINA SHUSHO,MARTHA MWAIPAJA KUIYUMBISHA ARUSHA LEO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *