Album | William Otuck – ZAWADI YA KRISMASI | Download

Album mpya ya Krismasi!

Huu ndiyo wimbo wa utambulisho kutoka kwa William Otuck: https://mkito.com/song/zawadi-ya-x-mas/4691


Krismasi
hii, Santa hatokuwa akitoa zawadi peke yake. Na hata hivyo inaonekana
kuwa baadhi watamzidi katika hilo linapokuja suala la muziki! Otuck
William, muimbaji wa soul, athibitisha hilo kwa kuleta mbele yako bidhaa
mpya itakayobadili sura nzima ya msimu wa Krismas mwaka huu kimuziki.
Ni santuri itakayokuwa imebeba nyimbo kumi na tano (15) mahususi kabisa
kwa ajili ya Krismas.

Akizungumzia
album hiyo Otuck anasema; ““Zawadi Ya Krismasi” ni album yenye nyimbo
15 iliyotayarishwa kwa ushirikiano wa kwangu mwenyewe na Nach B,
mtayarishaji kutoka studio za Beats Bank Music zilizopo jijini Mbeya.
Hii si album ya dini (Gospel) japokuwa imebeba baadhi ya nyimbo za
zamani za kidini za Krismas, ambazo tumezitayarisha katika mahadhi
tofauti kidogo, lakini ni album inayohusu Familia, Matumaini, Faraja,
Imani na Upendo. Kwa kadri ya ufahamu wangu inaweza kuwa album ya kwanza
kabisa ya Krismas kuwahi kutengenezwa Tanzania au Afrika Ya Mashariki
kwa ujumla”.

Ni
wazi kwamba kila mtu anatamani kujua nini hasa Otuck ametuandalia,
kitakachodumu kwa muda mrefu na kutufariji kila ifikapo msimu kama
huu.  Album hiyo itakuwa ikipatikana katika mtandao wa Mkito.com kuanzia
Tar 26 Novemba 2014. Lakini pia itauzwa katika mfumo wa CD.

Kwa mawasiliano zaidi ya namna ya kupata CD hizo au kuwa wakala wa usambazaji, andika barua pepe kwa [email protected] au piga simu nambari +255712168011
Huu ndiyo wimbo wa utambulisho: https://mkito.com/song/zawadi-ya-x-mas/4691

Social Media:

Twitter: @Otuck_William

Instagram: @Otuck_William
https://mkito.com/song/zawadi-ya-x-mas/4691/bwi-1-7182
Twitter: @djmwanga     
Instagram: @djmwanga     
Facebook Fans Page: DJMwanga