POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?

POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?

KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASURI SHOW TANGU SAA 4 USIKU

PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! HAIBU

Stuttgart,Ujerumani,

Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri

Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake,

Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki

ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa

wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika “Washabiki wa hasira nawe DIAMOND” link: BONYEZA HAPA

 
 Huu ndio ukumbi uliharibiwa na washabiki mjini stuttgart,ujerumani
ad

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *