THE RETURN OF CHAIR OWNER | Alikiba – Mwana&Kimasomaso | Download

Baada ya wapenzi wa muziki
Tanzania kusubiri kwa muda mrefu sasa wamepata nafasi ya kujiburudisha na ngoma
mpya kutoka kwa Alikiba. Tarehe 25 Julai, 2014 Alikiba ameachia single mbili
mpya kwa wakati mmoja ziitwazo “Mwana” na “Kimasomaso”. Alikiba anajulikana
ndani na nje ya Tanzania kwa hit zake kama Cinderella, Mapenzi yanarun dunia,
Single boy, na Dushelele. Cinderela ndiyo wimbo ambao mpaka sasa umeweka rekodi
ya kuuza copy nyingi katika Afrika Mashariki mwaka 2008. Mwaka 2012 Alikiba
alishinda tuzo ya best Rhumba/ Zouk na wimbo wake wa “Dushelele” katika tuzo za
Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Alikiba anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa
kuimba na utunzi wa nyimbo pamoja na kuwa mburudishaji mkali sana katika show
zake za live na mpaka sasa ametembea nchi nyingi sana duniani kuburudisha
wapenzi wa muziki. Sasa unaweza kupata nyimbo mbili mpya za Alikiba bure katika
tovuti ya www.mkito.com

Alikiba – Mwana

https://mkito.com/song/mwana/2195/bwi-1-177
Alikiba -Kimasomaso

https://mkito.com/song/kimasomaso/2194/bwi-1-188

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *