New Music From Otuck. Video and Audio (Deja Vu Ft. Hance Puff)

 OTUCK: “Utabibu unanisaidia kufanya muziki mzuri”Muziki
mzuri hutengenezwa kwa ustadi wa mchanganyiko wa ala za sauti na
mashairi. Sanaa ya utengenezaji muziki mzuri ni kazi ambayo
watayarishaji na wasanii kwa pamoja huifanya wakati wa utengenezaji wa
wimbo. Mara nyingi, wasanii na watayarishaji wa muziki hutengeneza
muziki kutokana na mazingira halisi yanayowazunguka katika maisha yao
binafsi kama vile maisha ya mapenzi, kazi nk.


Otuck William, msanii mpya kwenye maskio ya wapenzi wengi wa
muziki nchini ambaye pia ni Afisa Tabibu, anaelezea namna ambavyo kazi
yake ya utabibu imechangia katika utengenezaji wake wa muziki.

“Siku
yangu ya kawaida kwa kiasi kikubwa naitumia kusikiliza wagonjwa na
wateja wengine wanaokuja kwenye kituo cha afya ninachofanyia kazi. Ni
kitu ambacho ninakipenda maana kinanipa nafasi ya kusaidia jamii.
Imekuwa ni ndoto yangu kwa muda mrefu. Lakini pamoja na kusikiliza
matatizo yao ya afya, ukiwa mhudumu wa afya, watu hukuamini, wengi
watakueleza matatizo yao ya ndani sana ambayo pengine hawawezi kuwaambia
hata wapenzi wao, hivyo kuongea nao kila siku kunanipa nafasi ya
kujifunza mengi sana kuhusu watu na Maisha. Muziki ninaoufanya ni kwa
ajili ya watu na Maisha, hivyo yale nijifunzayo kwa watu niwaonao kila
siku, huwa ninajaribu kuyatafsi katika ala za muziki. Ni namna moja wapo
ya kutengeneza kitu ambacho kinawahusu watu moja kwa moja. Hivyo
kinakuwa bora na kizuri…” – Otuck William

Pamoja na kazi nyingi ambazo ziko studio, mwimbaji huyu wa
Soul anafanya vizuri kwenye vituo mbali mbali vya TV na Redio kupitia
rekodi yake iitwayo “Deja Vu” ambayo imetayarishwa na yeye mwenyewe na
video imeongozwa na kutayarishwa na Nikki Dizzo wa Focus Film Tanzania.


Kama bado hujapata nafasi ya kuangalia Video hiyo, hii hapa   

Lakini pia unaweza kupakua audio ya deja vu kwenye mtandao wa soundcloud.

https://soundcloud.com/otuckwilliam/deja-vu-otuck-william-ft-hance-puff