[NewZ] Wimbo mpya wa Ngwair ‘Alma’ kuachiwa rasmi siku ya Valentine mwaka huu, una story ya kweli

Ikiwa ni miezi nane imepita tangu afariki mkali wa mitindo huru,
Albert Mangwea aka Ngwair, wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Alma
unatarajiwa kuachiwa rasmi February 14, 2014 ambayo ni siku maalum ya
wapendanao (Valentine’s day).

Akiongea na tovuti ya DJMwanga.com, Muro ambaye ni moja kati ya
wasimamizi wa kazi za Albert Mangwea ambaye anaisimamia project ya wimbo
huo, amesema kuwa wimbo huo uliorekodiwa ndani ya studio za AM Records
utaachiwa rasmi siku ya Valentine na kwamba anaendelea kuwasiliana na
familia yake kuhusu mapato ya wimbo huo ambayo atapewa mama yake Ngwair.

“Yeye alitaka kuitoa ngoma hiyo siku ya Valentine mwaka jana, kwa
hiyo na mimi nimeamua kuitoa siku hiyo hiyo. Niliongea na Familia
Morogoro, na ntawapigia tena ili tuangalie tunachofanya kwa sababu kuna
vitu vingi vya kuconsider, kuna mambo ya ringtones na nini na nataka
nizungumze pia na makampuni ya simu. Kwa sababu kila alichotakiwa apate
yeye (Ngwair) inabidi apate Mama yake.” Muro ameiambia tovuti ya DJMwanga.com.

Muro ameeleza kuwa wimbo huo wenye ujumbe wa mapenzi unazungumzia
story ya kweli na ulikuwa maalum kwa mtu wa karibu wa marehemu Ngwair,
“Kila kitu alichokuwa anakiimba kilikuwa cha ukweli, ni true story.”

January 16, 2013, Ngwair mwenyewe alitangaza kuwa ataachia wimbo huo
siku ya Valentine (February 14, 2013) ambao alidai ni zawadi ya
Valentine kwa fans wake na wimbo huo ulikuwa kwenye album yake iitwayo
MIMI 3, lakini baadae aliahirisha na kuachia wimbo wa ‘Beef’ akiwa na
TID.

Muro amesema kuwa kuna matatizo yalitokea wakati huo ambayo marehemu
Ngwair hakupenda kuyazungumzia ambayo yalisababisha yeye kuahirisha
kutoa wimbo huo.

UtauPata Hapa Hapa DJMwanga.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *