MSANII WA LAST WARNING AKWAA TUHUMA NZITO JUU YA JOH MAKINI.

 
Msanii wa kundi La  Last Warning,  Inno Mtoa  Lock ameingia kwenye tuhuma 
kubwa  kutoka kanda ya kaskazini baada ya kuachia ngoma yake wiki mbili  zilizopita inayokwenda kwa jina  la nilivyomkuta  dar  ambayo amemshirikisha jamaa  toka kundi la jambo squad ambaye ni  jogoo kichaa a.k.a ordinary na kazi ikiwa imetengenezwa pale Noiz  Mekah ,producer akiwa Dx kuwa huo wimbo ni dongo la moja kwa moja kwa msanii Joh Makini Mwamba Wa Kaskazini .

akihojiwa katika interview ya radio moshi fm katika kipindi cha the base show ambacho huwa kinaanza saa saba hadi saa kumi kamili jioni  , mtoa lock alikumbana na wakati mgumu sana baada ya wadau na wasikilizaji wa hiyo radio waliotaka kujua ukweli kutoka kwake kuhusiana  na habari zilizozagaa  mitaani kuhusiana  na ngoma hiyo kuwa ni  dongo kwa Joh Makini Mwamba Wa Kaskazini .

wasikilizaji
walitaka ufafanuzi juu ya ngoma hiyo na madai kuwa ni kweli ni dongo
kwa msanii Joh Makini au ni habari tu. msanii huyo hata hivyo alionekana
kushtushwa na swali hilo na kushindwa kutolea ufafanuzi  wa kina juu ya wimbo huo na badala yake alisema ni wimbo tu ambao upo hivyo na wala si kweli kuwa amempiga dongo Joh Makini.      

                                      Joh Makini

hata hivyo blog ya DJMwanga.com ilipoamua kumtafuta Mtoa Lock  juu
ya kile kilichojiri katika interview yake hiyo, alisema yeye mwenyewe
hajui kinachoendelea juu ya tuhuma hizo na alishangazwa sana na maswali
hayo ambayo yalikuja mfululizo katika interview yake ambayo yalimtaka
atolee ufafanuzi juu ya madai hayo.

“patty katika kitu ambacho kilinishtua na kunishangaza ni juu ya maswali yaliyokuja mfululizo yakituhumu kuwa wimbo wangu wa “nilivyomkuta dar”, ambao nimeuachia hivi karibuni kabla ya sikukuu ya christmass kuwa nimemlenga Joh Makini Mwamba Wa Kaskazini  ,kitu ambacho sio kweli, nani  idea tu ya wimbo na style zetu kama  last warning.”alisema Mtoa Lock.

 wimbo wa Nilivyomkuta Dar, ambao una wiki  ya pili tangu uachiwe umekuwa gumzo kanda ya kaskazini naukizidi kuwa na tuhuma kwa  msanii wa ngoma hiyo Inno Mtoa Lock,kwamba amemuimba Joh Makini msanii ambaye anafanya poa sana katika gemu la hip hop ambapo anatoka kundi la weusi.
baadhi ya mashairi yaliyopo katika ngoma hiyo:
nilivyomkuta dar, kachaa  wa kitaa

alikuwa gangstar  aisee, sasa pang’ang’a balaa,

alikuwa ananyoa dongo,sahivi nywele kafuga,

midosho ya kibongo,hana modo za kichuga,

katekwa na mabishoo,katema pigo za huku

hachezi ngaleloo ye ni bingwa wa viduku………………

anasema anaswaga ,wazazi amewatupaga , jiji limemtekaga,

anapenda vizaga,

anasema arusha siji kula viporo.
UnaweZa IdownLoad Hapa Hii Track UisikilIze 
http://old.hulkshare.com/dl/q8j233rw8fsw/MtoaLock_ft_Ordinally-Nilivyomkuta_Dar__By__DJMwanga.com.mp3?d=1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *