DAYNA AFUNGA MWAKA KWA KUTOA MSAMAHA NA SHUKRANI ZAKE

Habari
zenu ndugu. Kwanza napenda kumshukuru mwenyezi mungu anayetupa pumzi
bila malipo, kwani yeye ndiyo kila kitu. Naishkuru familia yangu kwa
kunipa moyo kila kukicha mpaka hapa leo hii. Napenda kutoa shukrani
kwenu ndugu zangu kwa kunisapot katika
kazi zangu na ushauli wa kila leo. Tunakutana na mitihani mingi sana
lakini mungu anawapa moyo wa kuwa nami pamoja. shukrani sana kwa vyombo
mbalimbali vya habari kwa mwaka mzima kuendelea kunisapot kwa kila hali.
Radio na Tv mbalimbali kwa kutenga muda wa kupiga nyimbo zangu na
kunipa interview juu ya kazi zangu. nawashkuru sana . Studio mbalimbali
kwa kuweza kunipa nafasi ya kufanya kazi katika studio izo. Pia Bloggs
na website na Magazeti mbalimbali, mmtenga muda wenu kwa kuthamini kazi
za Dayna Nyange mmeonesha ushirikiano mkubwa sana kwangu. niwashukuru
waandaaji wa matamasha kwa kunipa nafasi ya kufanya show katika
matamasha hayo, ni jinsi gani mnavyoonesha kujali kazi zangu na kunipa
moyo. Lakini pia watangazaji na ma dj wa Radio husika mmekuwa mkitenga
muda wa kuwa nami katika kazi zenu,Niwashkuru sana Ma requester wote
Tanzania na nje ya Tanzania kwa ku request nyimbo zangu na kupata nafasi
ya kupigwa katika media izo. Nyinyi ni mchango mkubwa sana kwa sanaa
yetu .Mafans wangu mnaozidi moyo na kunishauli juu ya kazi zangu na
maisha kwa jumla kupitia vyanzo vyangu vya mawasiliano. Tunafunga mwaka
2013 na tunaamia mwaka 2014 Sitawaangusha.. Mwaka 2013 , tumepoteza
ndugu zetu tuliokuwa nao ktk tasnia hii. Tuzidi kumuomba mungu
azipumzishe roho zao mahali pema Albert mangwea, Langa kileo, marc malim
Sharomilionea, Sajuki,na wengine wote wapumzike kwa amani. Nichukue
nafasi hii kuomba radhi kwa wote niliowakosea au kukoseana kwani ni
madhaifu ya kibinaadam. Lakini pia niseme tu kwa wote walionikosea
Nimewasamehe bila kinyongo chochote na kwa dhati toka moyoni mwangu.
Tusahau yaliyopita tuanze mwaka tukiwa Safi. Tumuombe mungu atupe afya
njema na mafanikio zaidi mwaka 2014 na Kuendelea. Amina.

By
Dayna nyange

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *